Faida za kula bagia
Faida Za Kula bagia(Andazi la dengu/lentils Andashi)
Kila kiumbe kitazeeka,lakini haimaanishi usitumie lishe mbalimbali kuendekea kuwa na Afya njema.
Dengu au Aina maharage,hupatikana Kwa wingi karibu kila eneo DUNIAni,Kuanzia Bara la Mtu Mweusi-AfroNationa/Africa, America Kaskazini, America Kusini,Ulaya,Russia/ardhi ya mihama ya kirusi(land of Russia date palm trees Hadi Australia/ardhi ya Kondoo.
Dengu njano au rangi inginezo ni zao linalopatikana Kwa kulimwa,Lina lishe hizi mwilini
-madini Chuma
-protini
-potasium
-nyuzinyuzi(fiber)
-seleniam
-folate
-Nguvu
-Wanga
-mafuta
-calcium kidogo
Dengu njano,huandaliwa kama lishe Bagia,Kisindikizi chakula(Mboga) na Mkate Kwa baadhi ya Maeneo Katika Sayari DUNIA,Leo Tutaongelea faida ya Kula Bagia.
Ukipenda kukaa alipo mtaalam wa KUANDAA pishi Bagia huweka unga wa dengu laini,hamira,chumvi,kitunguu Maji,Mchicha kidogo au spinach na Kiongeza harufu,Wengine huweka na unga wa Ngano kidogo na hulainishwa Kwa Maji Vuguvugu,Kisha hukoroga iwe na Uzito kama Uji hivi mzito na huiacha hamira ifanye kazi mithili ya Saa Moja.
Baada ya hapo Huchota kidogo na Kukaanga Kwa mafuta mengi ya Alizeti,Mafuta mazito au ya Mawese ,Ila wengi hupendelea Alizeti.
Sehemu zinginezo DUNIAni hukandwa na kuokwa kama Mkate badala ya Kupika Kwa mafuta mengi kama Bagia,huita Mkate wa dengu,Lentils bread.
Baadae mapishi hutumiwa pamoja na Kachumbari,Chai au Kinywaji Laini.
FAIDA YA KULA BAGIA ZA DENGU
1-Inapunguza kupata Magonjwa Baadhi ya kudumu
Tafiti baadhi husema hupunguza uwezekano wa magonjwa kama vile Kisukari,Saratani,Shambulio la moyo na Unene kupindukia,hii ni kutokana na wingi wa Lishe phenols ndani yake.
2-Inasaidia kusagwa Kwa Chakula tumboni
Hii ni kutokana na nyuzi nyuzi(fibre) ambazo huweka mazingira mazuri Kwa Tumbo kusaga na kulainisha chakula.
3-Kulinda afya ya Moyo
Dengu Zina wingi wa nyuzinyuzi, potassium, vitamin B1 na Madini Chuma lishe ambazo husaidia mishipa ya Moyo na Kulinda Mizunguko wa damu .
4-Inasaidia kuweka sawa kiwango Cha Sukari
Vyakula jamii ya mikunde,ikiwemo dengu,Huwa na nyuzinyuzi nyingi ambazo huthibiti hamu ya Kula na kusababisha Mwili utumie Sukari Kwa usahihi.
5-Ni chanzo Cha Protini ya mimea
Japokuwa kila mtu atazeeka kutokana na Mwili kufikia hatua ya kushindwa kutumia protini iliyomo mwilini, Matumizi ya protini itokanayo na mimea yanashauriwa kuwa mazuri kuliko ile ya vyakula-damu(Nyama) Kwa kuwa huaminika ni haraka zaidi kupokelewa na Mwili,Inafaa sana Kwa Ukuaji wa mtoto,Kuanzia umri wa miaka 6 pia hufaa sana Kwa wanaopendelea kusoma ,Pia walioko maofisini,ni Protini nzuri Kwa ubongo wa Kati.
,
Kupata Lishe ya ZIADA Kwa afya yako na Tiba ya matatizo mbalimbali wasiliana na Laurian 0655858027 au promota927@gmail.com au afyaraha@gmail.com
Mawasiliano Toka AfyaRaha Tanzania
Comments
Post a Comment